Sunday, August 29, 2010

076

076

Watu huzaliwa teketeke na laini;
Wafu, ni wagumu na waliokakamaa.
Mimea huzaliwa mororo na inayojikunja;
Ikinyauka, huwa inasagika na kavu.

Kwa hiyo yeyote anayekakamaa na kutokunjika ni mfuasi wa mauti.
Yeyote anayelainika na kuteleza ni mfuasi wa uhai.

Kilicho kigumu na kilichokakamaa kitavunjika.

Kilicho kilaini na teketeke kitadumu daima dawamu.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010
Kwa jinsi inavyofanya kazi yake hapa duniani, Tao hii ni kama vile upinde,
Sehemu ya juu inajipinda kuelekea chini; na sehemu ya chini inajipinda kuelekea juu.
Hurekebisha kati ya ziada na upungufu ili pawe na mlingano sadifu.
Huchukua toka kwa kile kilichozidi na hutoa kwa kile kilichopungua.

Wanaotaka kudhibiti na kutumia nguvu ili kulinda mamlaka yao;
daima huwa wanakwenda kinyume cha mwelekeo wa Tao.

Maana huwa wanachukua kwa wale walioshiwa na kuwapa wale waliovimbiwa.

Gwiji huweza kutoa daima kwani utajiri wake hauna ukomo.
Hufanza bila matarajio; na hufanikiwa bila kutaka kusifiwa na kukuzwa,
na hakuna siku hata moja anayojiona yeye ni bora kuliko wengine.

078

Hakuna kitu chochote duniani laini kama maji unapoyashika.

Lakini unapotaka kulainisha vigumu na visivyokunjika hakuna zana bora kama maji kwa kazi kama hiyo.

Laini hushinda kigumu;
na mororo hushinda kilichokakamaa.
Kila mtu anajua hili ni kweli; lakini wachache sana wanaoweza kulifanza hili kwa matendo.

Kwa sababu hii ndiyo maana gwiji huwa mtulivu wakati wa majonzi.

Ushetwani hauingii moyoni mwake.
Kwa kuwa alishaghairi kusaidia, basi huwa ndiye msaada mkubwa kabisa kwa watu.

Maneno haya budi yanaonekane yanayojikinza. [Kwa wasiojua].


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

078

078

Hakuna kitu chochote duniani laini kama maji unapoyashika.

Lakini unapotaka kulainisha vigumu na visivyokunjika hakuna zana bora kama maji kwa kazi kama hiyo.

Laini hushinda kigumu;
na mororo hushinda kilichokakamaa.
Kila mtu anajua hili ni kweli; lakini wachache sana wanaoweza kulifanza hili kwa matendo.

Kwa sababu hii ndiyo maana gwiji huwa mtulivu wakati wa majonzi.

Ushetwani hauingii moyoni mwake.
Kwa kuwa alishaghairi kusaidia, basi huwa ndiye msaada mkubwa kabisa kwa watu.

Maneno haya budi yanaonekane yanayojikinza. [Kwa wasiojua].


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

079

Kutokufaulu ni fursa ya aina yake.
Ukimlaumu mtu mwingine kwa kutofanikiwa, hakuna mwisho wa lawama.

Kwa hiyo Gwiji hutekeleza majukumu yake na kusahihisha makosa yake yeye mwenyewe.

Hufanya kile anachoweza kukifanya, na hahitaji chochote kutoka kwa watu wengine.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy

Makilla-2010

080

Nchi ikitawaliwa kwa busara, raia huridhika na kustawi.
Hufurahia matunda ya kazi za mikono yao na hawapotezi muda wao kugundua mashine za kuwarahisishia kazi.
Kwa kuwa hupenda mno nyumba zao, huwa hawana hamu ya kusafiri.
Panaweza kuwepo mabehewa na madau kadhaa, lakini hivi huwa haviendi popote.
Panaweza kuwa na lundo la silaha lakini kamwe hakuna anayezitumia wala kuwazia vita.
Watu hufurahia vyakula vyao, hufarajika kwa kukaa na familia zao, na hutumia napumziko yao kuhudumia bustani zao, hufuatlia kinachoendelea kwa majirani zao. Na licha ya kwamba nchi jirani iko karibu nao sana na watu wake wanaweza wakasikia majogoo yao yakiwika na mbwa wao wakibweka, wanatosheka na kufa hali wakiwa na umri mkubwa bila ya kwenda kuiona nchi hiyo jirani.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy

Makilla-2010

081

Maneno ya kweli si fasaha; na maneno fasaha si kweli.
Wenye busara hawahitaji kuthibitisha hoja zao; na watu wanaohitaji kuthibitisha hoja zao sio watu wenye busara.

Gwiji hana anachomiliki.
Kadri anavyowafanyia wengine hisani zaidi ndivyo anavyofurahi zaidi.
Kadri anavyowapa wengine, ndivyo anavyozidi kuwa tajiri.
Tao hulisha bila kulazimisha.
Bila kuwa mtawala wa kiimla, gwiji huongoza.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]