Kwa jinsi inavyofanya kazi yake hapa duniani, Tao hii ni kama vile upinde,
Sehemu ya juu inajipinda kuelekea chini; na sehemu ya chini inajipinda kuelekea juu.
Hurekebisha kati ya ziada na upungufu ili pawe na mlingano sadifu.
Huchukua toka kwa kile kilichozidi na hutoa kwa kile kilichopungua.
Wanaotaka kudhibiti na kutumia nguvu ili kulinda mamlaka yao;
daima huwa wanakwenda kinyume cha mwelekeo wa Tao.
Maana huwa wanachukua kwa wale walioshiwa na kuwapa wale waliovimbiwa.
Gwiji huweza kutoa daima kwani utajiri wake hauna ukomo.
Hufanza bila matarajio; na hufanikiwa bila kutaka kusifiwa na kukuzwa,
na hakuna siku hata moja anayojiona yeye ni bora kuliko wengine.
078
Hakuna kitu chochote duniani laini kama maji unapoyashika.
Lakini unapotaka kulainisha vigumu na visivyokunjika hakuna zana bora kama maji kwa kazi kama hiyo.
Laini hushinda kigumu;
na mororo hushinda kilichokakamaa.
Kila mtu anajua hili ni kweli; lakini wachache sana wanaoweza kulifanza hili kwa matendo.
Kwa sababu hii ndiyo maana gwiji huwa mtulivu wakati wa majonzi.
Ushetwani hauingii moyoni mwake.
Kwa kuwa alishaghairi kusaidia, basi huwa ndiye msaada mkubwa kabisa kwa watu.
Maneno haya budi yanaonekane yanayojikinza. [Kwa wasiojua].
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, August 29, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment