Sunday, August 29, 2010

080

Nchi ikitawaliwa kwa busara, raia huridhika na kustawi.
Hufurahia matunda ya kazi za mikono yao na hawapotezi muda wao kugundua mashine za kuwarahisishia kazi.
Kwa kuwa hupenda mno nyumba zao, huwa hawana hamu ya kusafiri.
Panaweza kuwepo mabehewa na madau kadhaa, lakini hivi huwa haviendi popote.
Panaweza kuwa na lundo la silaha lakini kamwe hakuna anayezitumia wala kuwazia vita.
Watu hufurahia vyakula vyao, hufarajika kwa kukaa na familia zao, na hutumia napumziko yao kuhudumia bustani zao, hufuatlia kinachoendelea kwa majirani zao. Na licha ya kwamba nchi jirani iko karibu nao sana na watu wake wanaweza wakasikia majogoo yao yakiwika na mbwa wao wakibweka, wanatosheka na kufa hali wakiwa na umri mkubwa bila ya kwenda kuiona nchi hiyo jirani.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy

Makilla-2010

No comments:

Post a Comment