Unaweza kuilazimisha akili yako kuacha kutangatanga na kurejea kwenye asili yake ya kuwa kitu kimoja ?
Je, uanweza kuufanya mwili wako uwe teketeke kama wa kitoto kichanga ?
Unaweza kuusafisha mwoneko wako wa ndani hadi unakuwa huoni kitu kingine ila mwanga ?
Unaweza kuwapenda watu na kuwaongoza bila ya wewe kutaka kuwaamlia kila kitu ?
Je, unaweza kuyashughulikia mambo yote muhimu kwa kuyaachia mambo yajiongoze yenyewe ?
Je, unaweza kuiacha nyuma akili yako ili uweze kuelewa kila kitu ?
Kuzaa, kutunza na kukimu,
kuwa nacho bila ya kumiliki,
kufanza bila kutarajia kitu,
kuongoza bila kudhibiti,
hakika hii ndio adili aali kuliko zote.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Tuesday, September 7, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment