Kuna wanaosema mafudisho yangu eti ni ujinga.
Wengine wanasema ni aali lakini yasiyotekelezeka.
Lakini kwa wale waliobahatika kujitazama ndani mwao;
huo ujinga una maana kamili inayoeleweka.
Na kwa wanayoyatia katika vitendo
huu uaali una mizizi inayoingia ndani sana.
Nina vitu vitatu tu vya kufundisha:
Kutokujiona, Uvumilivu na Huruma.
Hivi vitatu ni hazina yako iliyo bora kabisa.
Kutokujiona katika matendo na mawazo,
kunakurudisha kwenye chanzo cha kuwepo kwako.
Uvumilivu na rafiki na maadui zako unakubaliana na hali halisi kama ilivyo.
Huruma kwa upande wako mwenyewe, unapatanisha vitu vyote duniani.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Saturday, September 4, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment