Monday, September 6, 2010

030

Anayeitegemea Tao kuwatawala binadamu huwa halazimishi jambo lolote au kuwashinda maadui kwa kutumia uongo au dhuluma au silaha.
Kwa kila nguvu inayotumika kuna nguvu kama hiyo hiyo ikiipinga nguvu hiyo ya kwanza.
Vitendo vyote vya kutumia nguvu hata iwe kwa nia njema kiasi gani bado siku zote humgeukia mtumia mabavu.

Gwiji huifanya kazi yake ni kisha husimama.
Anaelewa kwamba ulimwengu milele haudhibitiki, na kwamba ukiritimba na kujaribu kutawala kila kitu huenda kinyume na mkondo wa Tao.
Kwa sababu mwenyewe anajiamini huwa hana muda wa kuwafanya wengine wamwamini.
Kwa sababu anaridhika na kile alicho hana sababu ya kupata ridhaa ya wengine.

Kwa sababu anajikubali yeye mwenyewe, basi dunia nzima inamkubali.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment