Mafanikio ni hatari kama vile kushindwa,
Matumaini hayana kina kama uoga usivyo na kina pia.
Ina maana gani kusema mafanikio ni hatari kama kutofanikiwa ?
Kama unapanda ngazi kwenda juu au kushuka chini nafasi yako wakati wote ni ya wasiwasi.
Unaposimama kwa miguu yako miwili,
wakati wote utakuwa na balansi ya uhakika.
Nini maana ya matumaini na uoga vyote kutokuwa na kina sana ?
Matumaini na uoga ni viinimacho ambavyo vyote hutokana na mtu kutanguliza kufikiria nafasi yake kuliko kitu kingine,
Tutakapoiona nafsi kama sio nafsi yetu tu je, kutakuwa na sababu ya kuogopa kitu chochote?
Ione dunia nzima kama ndiyo nafsi yako.
Kuwa na imani na mambo kama yalivyo.
Ipende dunia kama unavyoipenda nafsi yako,
kisha utaweza kuviangalia vitu vingine vyote.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Tuesday, September 7, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment