Saturday, September 4, 2010

070

Mafundisho yangu ni rahisi kuelewa na ni rahisi kuyatia katika vitendo.
Hata hivyo ubongo wako hauwezi kamwe kuyaelewa,
na ukijaribu kuyatia katika vitendo lazima utashinwa.

Mafundisho yangu ni ya zamani kuliko dunia.
Utawezaje kiumbe kuelewa maana yake ?

Ikiwa unataka kunijua mimi,
jiangalie ndani ya moyo wako.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment