Mito yote huelekea baharini
kwa kuwa iko chini kuliko ilivyo mto.
Unyenyekevu wake ndio huipa nguvu iliyokuwa nayo.
Ukitaka kutawala watu
ni lazima wewe ujiweke chini yao.
IKiwa unataka kuwaongoza watu,
ni lazima ujifunze jinsi ya kuwatii na kuwafuata.
Gwiji daima yuko juu ya watu,
na hakuna anayejisikia anakandamizwa.
Huwatangulia watu wake kwa kila jambo, na hakuna anayejisikia kwamba anatumiwa.
Dunia nzima huwa inamshukuru.
Kwa kuwa hashindani na mtu, hakuna anayeweza kushindana naye.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Saturday, September 4, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment