Monday, September 6, 2010

022

Ukitaka kuwa mkamilifu,
acha kwanza uwe vipande vipande.
Ukitaka unyooke,
acha kwanza upinde pinde.
Ukitaka uwe umejaa,
acha kwanza uwe tupu.
Ukitaka uzaliwe upya,
acha kwanza ufe.
Ukitaka upate kila kitu duniani,
acha kwanza utoe kila kitu ulicho nacho sasa.
Mwalimu anapokaa kwenye Tao,
basi huwa anakuwa mfano wa kuigwa na viumbe wote duniani.
Kwa sababu huwa hajioneshi,
basi watu huiona nuru yake.
Kwa sababu hana chochote cha kuthibitisha,
basi watu wanaamini maneno yake.
Kwa sababu hajijui yeye ni nani,
watu hujitambua wenyewe kupitia kwake.

Kwa sababu akilini hana malengo yoyote,
kila kitu anachofanya hufanikiwa.

Walimu wa zamani waliposema:
" UKitaka upate kila kitu, basi achia kila kitu, "
hawakuwa wakisema maneno matupu.
Ni pale unapoishi kama Tao tu ndipo unapoweza kuwa kweli ni wewe mwenyewe na sio kinyago cha Mzungu, Mmarekani, Mwarabu, Mchina au mtu mwingine au nyani mtu kwa wengine.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment