Saturday, September 4, 2010

061

Nchi moja inapokuwa na nguvu sana duniani, hushabihiana na bahari.
Mito na vijito vyote hutiririsha maji yajaye humo.
Kadri inavyokuwa na nguvu zaidi ndivyo inavyopaswa kuwa na unyenyekevu zaidi.
Unyenyekevu una maana ya kuiamini Tao zaidi,
hivyo kutokuwa na haja ya kujihami.

Taifa kubwa ni kama vile mtu maarufu,
Anapofanya kosa haraka hutambua makosa yake.
Anavyotambua kafanya kosa hukiri kufanya kosa.
Akishakubali kosa lake haraka hujisahihisha.
Huwahusudu na kuwathamini wale wanaoonyesha udhaifu wake
kwani huwachukulia kama walimu wake walio wema sana kwake.
Huwachukulia maadui zake kama kivuli chake mwenyewe.


Taifa huwa limejikita kwenye Tao
pale linapowaruzuku vyema watu wake na haliingilii mambo ya watu wengine,
litakuwa ni mwanga kwa mataifa mengine duniani.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment