Saturday, September 4, 2010

074

IKiwa utamaizi kila kitu hubadilika, hakuna utakachojaribu kuking'ang'ania.
Kama haugopi kufa,
hakuna utakachoshindwa kukifanya.

Ukijaribu kuidhibiti akheri,
ni kama kutaka kuchukua nafasi ya seremala gwiji.
Ukizishika zana za serelamala gwiji, uwezekano ni kuwa lazima utajikata mkono wako.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment