Tao inasambaa kote.
Vitu vyote huzaliwa kutokana nayo, ingawa siyo inayoviumba,
Hujizatiti katika kazi yake,
lakini haina madai yoyote.
Huzilisha dunia nyingi tu, lakini haizimiliki.
Kwa kuwa inaungana na dunia zote na kujificha katika mioyo yao inaweza ikaitwa yenye nyenyekevu.
Kwa kuwa vitu vyote huishia ndani yake, nayo pekee ndiyo inayobakia
inaweza kutukuzwa na kuitwa maarufu.
Haina habari na umashuhuri wake, na hivyo kwa kweli ni maarufu sana.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment