Sunday, September 5, 2010

050

Mwalimu huwa anajitolea kwa lolote lile linalokuja mbele yake wakati wowote.
Anajua alizaliwa na atakufa,
na hakuna atakayemnusuru na hilo:
Hana kinachomdanganya akilini mwake
na hakuna kizuizi katika mwili wake.
Hakai kufikiria kile anachokitenda
Maana matendo yake huwa yanatiririka kwenye kiini cha ndani cha utu wake.
Huwa hazuii kitu chochote katika maisha yake;
Kwa hiyo yuko saa zote tayari kwa mauti.
Kama mtu anavyokuwa tayari kwenda kulala
baada ya kazi nzuri kwa siku hiyo.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment