Monday, September 6, 2010

035

Yule anayejikita kwenye Tao anaweza kwenda mahala popote anapotaka bila kuogopa hatari yoyote.

Huuona umoja wa dunia, hata katika adha na maumivu makubwa kiasi gani,
kwa sababu ameshaipata amani katika moyo wake.

Muziki na harufu ya chakula kizuri huwenda vikawasimamisha watu kwa muda wakavifurahia.
Ila maneno yanayoelekeza watu kwenda kwenye Tao yanaonekana ni yale yale yanayojirudia na hayana ladha tamu.
Ukiitafuta huna utakachokiona.
Ukijaribu kuisikiliza huna utakachokisikia.
Ukiitumia, basi huwa haiishi.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment