Jieleze kwa ukamilifu, na kisha kaa kimya.
Kuwa kama vile nguvu za maumbile:
upepo ukipuliza, upo tu upepo;
mvua inaponywesha; ipo tu mvua;
mawingu yakishapita
basi jua huonekana.
Ukifungua moyo na akili zako kwa Tao,
wewe unakuwa ni mmoja na Tao,
na unaweza kuikumbatia yote kikamilifu.
Ukifungua moyo na akili yako kwa mitazamo ya ndani na nje;
basi unakuwa wewe mwenyewe mtazamo wa ndani na wa nje,
na unaweza ukalitumia hili kwa ukamilifu.
Unapofungua moyo na akili zako kwa hasara, unakuwa ni kitu kimoja na hasara na utalikubali hili moja kwa moja.
Ifungulie Tao sasa,
na kisha amini, fuata akili yako ya kuzaliwa na utajikuta unakiacha kila kitu mahala kinapostahili kuwepo.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment