Tuesday, September 7, 2010

011

Huwa tunaziunganisha spoki na gurudumu lakini ni tobo lililopo katikati ndilo linalolifanya gurudumu kutembea.

Huwa tunatengeneza vyungu kwa umbo la duara na nje kukapendeza sana,
lakini ni shimo tupu lililo katikati ndilo lenye thamani na ndilo linalohifadhi humo ndani chochote kile tunachotaka kukihifadhi.

Tunatumia miti au mbao pamoja na mawe na matofali kujengea nyumba.
Lakini kinachohitajika ni nafasi iliyomo ndani ya nyumba ili kuishi humo ndani.

Huwa tunafanya kazi na vilivyopo lakini ni vile visiopo ndivyo tunavyovitumia.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]

No comments:

Post a Comment