Monday, September 6, 2010

039

Katika umoja na Tao mbingu ziko wazi na zina nafasi kubwa na ya kutosha,
Ardhi ni ngumu na iliyojaa,
Viumbe wote hustawi pamoja,
Wote wakiridhika kwa namna walivyo,
Daima dawamu wakijirudia wao wenyewe, bila mwisho wakizaliwa upya.

Mtu anapoiingilia Tao,
Anga hugeuka kuwa chafu,
Na ardhi huwa mashimo maltupu
Uwiano huporomoka
na viumbe hutoweka.

Mwalimu huangalia kila sehemu kwa huruma
kwa sababu anaelewa kilicho kizima.
Matendo yake ya kila siku ni unyenyekevu.
Hang'ari kama kito bali huiachia Tao kumuumba na kumfanya alivyo, asiye na umbo wala ulaini kama vile mawe ya kawaida.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment