Anayesimama kwa vidole vyake vya mguu hawezi kuliweka umbo lake sawa.
Anayekimbilia kutaka kwenda mbele zaidi , huwa haendi popote.
Anayekazana kung'ara na kuwashinda wengine huwa anafifisha mng'ao na nuru yake.
Anayejaribu kujieleza kuwa yeye ni nani hawezi kujua yeye ni nani hasa.
Aliyekuwa na mamlaka juu ya wengine, hawezi yeye mwenyewe kujipa nguvu na uwezo juu ya chochote.
Anayeng'ang'ana tu na kazi yake, hawezi kuunda chochote cha maana kitakachodumu duniani.
Ukitaka kuwa kitu kimoja na Tao,
Timiza wajibu wako, kisha sahau ulichokifanya na ondoka nenda zako.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment