Tao huzaa Moja.
Na Moja huzaa Mbili.
Mbili huzaa Tatu.
Na Tatu huzaa vyote vilivyomo duniani.
Vitu vyote vinaupa mgongo jinsia ya kike na husimama kuelekea jinsia ya kiume.
Jinsia ya Kike na Kiume zikichanganyika maelewano na amani hupatikana.
Mtu wa kawaida huchukia Utawa.
Mwalimu anaupenda na kuutumia, akakumbatia upweke akijua fika kwamba wakati huo yeye ni mmoja na ulimwengu wote.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment