Kitu kizito ndio mzizi wa kilicho chepesi,
Kisichotembea ndio mwanzo wa mienendo yote.
Ndiyo maana Mwalimu husafiri siku nzima bila kuondoka pale alipo.
Licha ya uzuri wa vile vinavyomzunguka siku nzima huwa katulia alipokaa.
Kwanini Bwana wa nchi awe na kiherehere na kujirahisisha kama mjinga ?
Ukijiachia ukawa unapeperushwa mbele na nyuma hujikuta huna mizizi yoyote.
Ukiafiki, kutotulia kuanza kukutembeza huku na huko basi utapoteza mawasiliano na kile wewe ulicho. Hutokuwa ni wewe mwenyewe ila kitu kingine kabisa.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment