Magwiji wa kale hawakujaribu kuwaelimisha watu, ila kwa wema kabisa waliwafundisha kutokufahamu.
Watu wanapofikiri kuwa tayari wanajua majibu ya mambo yote wanakuwa wagumu kuelekezwa.
Wanapokuwa wanajua kuwa hawajui inakuwa ni rahisi kwa watu kujiongoza wao wenyewe.
Ikiwa unataka kujifunza kutawala, epuka kuwa mwenye akili sana au tajiri.
Mfumo rahisi kabisa ndio ulio dhahiri na wazi zaidi.
Tosheka na maisha ya kawaida,
unaweza kumuonesha watu wote njia ya kurudi kwenye asili yao ya kweli.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Saturday, September 4, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment