Monday, September 6, 2010

031

Silaha ni zana za maangamizi na watu wote wema huzichukia.

Silaha ni vifaa vya kuwatisha na kuwaogopesha watu, na kila mtu mwema hatozitumia isipokuwa pale ambapo haiwezekani kuacha kufanya hivyo,
na akilazimika kuzitumia, huzitumia kwa uangalifu mkubwa na kwa uzito na majonzi makubwa moyoni.

Amani ndicho kitu bora zaidi na cha thamani kubwa kabisa.
Amani ikitoweka ni vipi yeye ataridhika ?
Maadui zake si mazimwi, ila tu watu kama yeye mwenyewe alivyo.
Hawatakii mabaya.
Wala haushangili ushindi dhidi yao.

Atakuwaje na furaha ya ushindi na uchinjaji watu kama yeye ?

Huingia vitani kwa huzuni,
majonzi mengi na huruma kama vile mtu aendavyo mazishini.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment