Saturday, September 4, 2010

062

Tao ndio kitovu cha ulimwengu,
hazina ya mtu mwema,
na hifadhi ya mtu mwovu.

Nishani huweza kununuliwa kwa maneno mazuri,
na heshima hupatikana kwa matendo mema;
Lakini Tao imezipita thamani zote,
na hakuna amayeweza kuipata.

Kwa hiyo, kiongozi mpya anapochaguliwa usijitolee kumsaidia kwa mali yako au kwa utaalamu ulio nao.
Badala yake jitolee kumfundisha nini maana ya Ta0.

Kwanini watu wa kale waliheshimu sana Tao ?
Kwa sababu ukiwa miongoni mwa wenye kuienzi Tao
Ukitafuta hupata;
na unapofanya kosa husamehewa.
Hii ndio sababu kila mtu anaipenda Tao.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment