Sunday, September 5, 2010

059

Hakuna kilicho bora katika kutawala nchi kama vile kiongozi kuwa mtu wa kiasi.

Alama ya mtu wa kiasi ni ile ya mtu kuwa huru kutoka fikira zake mwenyewe.
Mvumilivu kama mbingu,
Na anayepenya kila kitu kama vile miale ya jua,
Imara kama mlima
Na mwepesi kama mti kwenye kimbunga,
Hana kwa wakati huo anakokwenda,
Na huridhika kutumia chochote anacholetewa na maisha.

Hakuna kinachoshindikana kwake.
Kwa sababu ameachia kila kitu anaweza kuiangalia jamii nzima kama vile mama anavyomtunza na kumlea mwanawe.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment