Monday, September 6, 2010

028

Mfahamu mwanamme,
lakini kuwa pia na mwanamke:
Ipokee dunia nzima mikononi mwako
Ukiipokea dunia basi Tao haitaondoka tena kwako nawe utakuwa kama mtoto mdogo.

Ijue rangi nyeupe,
lakini bakia na rangi nyeusi.
Kuwa mfumo kwa dunia,
Ikiwa wewe ni mfumo kwa dunia basi Tao itakuwa imara ndani yako na hakuna chochote utakachoshindwa kukifanya katika dunia hii.

Yajue yale ya kibinafsi,
lakini bakia na yale yasiyo na mahusiano na yeyote:
Ipokee dunia kama ilivyo
Na kama utaikubali dunia basi Tao itakuwa ikiwaka ndani yako na utarejea kuwa kile unachostahili kuwa.

Dunia huumbwa kutoka kwenye ombwe,
kama vifaa kutoka kwenye pande la gogo.
Gwiji anavielewa vifaa na umuhimu wake,
lakini bado anabakia na gogo lake.
Kwa hiyo anaweza akatumia au kutengneza vitu vyote.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment