Monday, September 6, 2010

036

Ukitaka kukifanya kitu kiwe kidogo zaidi, lazima kwanza ukiachie kukua au kupanuka.
Ukitaka kukiteketeza kitu chochote ni lazima ukiachie kwanza muda wa kukua na kustawi.
Ukitaka kuchukua kitu chochote, lazima kwanza uwezeshe kitu hicho kutolewa.
Hili huitwa onekano yakinifu la jinsi mambo yalivyo.

Laini hushinda kigumu.
Na mwenda polepole humshinda mwenda mbio.
Fanya kazi yako iwe siri,
waoneshe watu kile ulichokwisha kukifanya.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment