Saturday, September 4, 2010

073

Tao sikuzote imo katika utulivu.
Hushinda bila ya kulazimisha,
hujibu bila kutamka neno hata moja,
huwasili bila ya kuitwa.
na hutekeleza bila kuwa na mpango.

Nyavu zake hugubika dunia nzima;
Na ingawa matundu yake ni mapana,
huwa haiachii hata kitu kimoja kuponyoka.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment