Mwalimu huwa hajaribu kuwa mtu mwenye nguvu au mamlaka,
Kwa hiyo ni mwenye nguvu na mamlaka kweli kweli.
Binadamu wa kawaida sikuzote hutaka kuwa na nguvu na vyeo zaidi;
Na kutokana na hili hata siku moja hawi na nguvu za kutosha wala hapati cheo cha kumridhisha.
Mwalimu kwa kawaida huwa hafanyi lolote,
Na bado huwa haachi lolote ambalo halijafanyika.
Mtu mwenye huruma hujitahidi kufanya chochote,
Lakini kunakuwa na mengi ambayo bado hayafanyiki.
Mtu muadilifu hufanya kitu fulani,
Lakini bado huwa anaacha mengi hayajafanyika.
Mtu mwenye utu hufanya kifu fulani, lakini pale anapoona hakuna kinachoendelea hukunja uso na mikono ya shati lake na kuanza kutumia nguvu.
Tao inapopotea basi wema hupatikana.
Wema nao unapopotea
basi utu huonekana.
Na utu unapopotea basi panakuwepo na mazoea.
Mazoea ni chuya za mazoea ya kweli,
Mwanzo wa vurugu na matatizo.
Kwa hiyo Mwalimu huwa anajishughulisha sana na vilivyo ndani zaidi na sio vilivyo juu au usoni.
Na tunda lenyewe na sio maua yake.
Hana dhamira binafsi.
Husihi katika uhalisia,
na huachia ndoto na mataminio yote kutoweka.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment