Tao haionekani.
Ndogo kuliko elektroni
na ndani yake ina dunia zisizo na idadi.
Kama wanaume na wanawake wenye nguvu wangelijikita kwenye Tao basi kila kitu duniani kingekuwa na upendo na amani.
Dunia ingelikuwa katika maridhiano.
Watu wote wangelikuwa katika amani, na sheria zote zingekuwa zimeandikwa katika mioyo yao.
Unapokuwa na majina na maumbo kumbuka hivi ni vitu vya muda.
Unapokuwa na taasisi weka mipaka ya mwisho wa shughuli zao.
Kujua wapi pa kuishia kutakusaidia kuepuka hatari na hasara nyingi.
Vitu vyote duniani huishia kwenye Tao, kama vile mito yote inavyoishia baharini.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment