Msafiri mzuri huwa hana mipango ya kudumu ma wala hana haraka ya kufika.
Mchoraji mzuri huachia hisia zake zimpeleke kokote kule zitakako.
Mwanasayansi bora huwa kajikomboa na dhana zote na kuacha akili zake wazi kukubali lolote lile liwalo.
Kwa hiyo Gwiji wakati wote ule anawakaribisha wote na hakuna anayemkataa.
Yuko tayari kutumia hali yoyote ile iwayo na hawi mbadhirifu kwa chochote kile.
Hili huitwa kuuvaa nuru yote.
Kwani mtu mzuri ni nani zaidi ya kuwa mwalimu wa mtu mwovu ?
Kwani mtu mbaya ni nani zaidi ya kuwa kazi ya mtu mzuri ?
Ikiwa wewe hulielewi hili basi lazima utapotea, hata ukiwa na akili kiasi gani.
Hili ni mama wa siri zote duniani !
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment