Majemedari wana msemo kwamba:
"Kuliko kuanza wewe kushambulia, ni bora zaidi wewe kusubiri na kuona.
Kulikoni kusogea hata nchi moja
ni bora kurejea nyuma hata kwa zaidi ya yadi moja.
Hili huitwa kusonga mbele bila ya kusogea mbele,
kurudisha nyuma bila ya kutumia silaha.
Hakuna nuksi kubwa kama kumdharau mpinzani wako.
Kumdharau adui yako ina maana kwamba wewe unaamini yeye ni mwovu.
Kwa hiyo unaziteketeza hazina zako tatu bora na kujigeuza wewe mwenyewe adui.
Pande mbili za wababe zikikutana kwenye kitali,
ushindi kwa kawaida huwa unakwenda kwa yule anayejua na anayekubali kushindwa.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Saturday, September 4, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment