Unataka kuiboresha dunia ?
Ninadhani hilo haliwezekani.
Dunia ni takatifu mno.
Haiwezi kuboreshwa na kiumbe.
Ukicheza nayo utaiharibu.
Ukiichukulia kama kitu basi utaipoteza.
Kuna wakati wa kuwa mbele, na kuna wakati wa kuwa nyuma;
Wakati wa kutembea na wakati wa kusimama;
Wakati wa kuchakarika, kutumia musuli na kumwaga jasho na wakati wa kuchoka na kupumzika;
Wakati wa kuwa salama na wakati wa kuwa katika hatari.
Mwalimu huyaona mambo kama yalivyo, bila ya kutaka kuingilia kati wala kuyadhibiti.
Huyaachia yafuate mkondo wake yenyewe, wakati akiishi katikati ya duara la Tao.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment