Kila aliyepandwa katika Tao
hawezi kung'olewa tena.
Kila anayekumbatia Tao hawezi tena kuteleza na kuanguka.
JIna lake litatukuzwa kwa hesima toka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Acha Tao iwe katika maisha yako ya kila siku nawe utakuwa mkweli na halisi.
Acha Tao iwe katika familia yako na familia yako itafaulu na kufanikiwa katika kila jambo.
Acha Tao iwe katika nchi yako na nchi yako itakuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine duniani.
Acha Tao iwe katika ulimwengu na ulimwengu utaimba.
Ninajuaje haya ni kweli ?
Ni kwa kuangalia kilichoko ndani mwangu.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment