Tuesday, September 7, 2010

015

Walimu wa kale walikuwa weledi na werevu mno.
Busara yao ilikuwa isiyo na kina.
Hakuna njia tunayoweza kuelezea, tunachoweza kueleza ni mwonekano wao wa nje tu.

Walikuwa waangalifu kama mtu aliyekuwa anakanyaga juu ya barafu iliyoko juu ya mto anaouvuka.
Waangavu kama askari katika nchi ya adui.
Wenye heshima kama wageni.
Majimaji kama barafu inayoyeyuka.
Inayoweza kuchongwa kirahisi kama kipande cha mti.
Kikaribishacho kama bonde.
Kinachoonekana wazi kama glasi ya maji.

Je, una subira ya kungoja mpaka tope lako limetulia na maji yamekuwa safi na meupe ?

Je unaweza kutulia hadi pale ambapo kitendo sahihi kinapoanza chenyewe ?

Mwalimu hatafuti kufanikisha mambo yake.
Na kwa kuwa hatafuti na hatarajii kitu chochote, yupo wakati wote na anaweza kukaribisha vitu vyote.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]

No comments:

Post a Comment