Sunday, September 5, 2010

048

Katika kutafuta elimu kila siku kuna kitu kipya kinachoongezwa.
Katika matendo ya Tao, kila siku kuna kitu kinachoondolewa.
Unahitaji kidogo na kidogo zaidi kuvilazimisha vitu, hadi hatimaye kufikia hali ya kutokufanya kitu.
Pale ambapo hakuna kinachofanyika,
basi sikuzote huwa hakuna kinachosahaulika kufanyika.

Ugwiji wa kweli hupatikana kwa kuachia mambo yajiendee yenyewe.
Hauwezi kupatikana kwa kuyaingilia mambo hayo.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment