Sunday, September 5, 2010

053

Njia hii kuu ni rahisi,
hata hivyo watu hupendelea vichochoro.
Tambua ni wakati gani mambo hayana ulingano. Jitahidi uwe katikati mwa Tao.

Walanguzi matajiri wanaponeemeka
Wakati wakulima wanadhulumiwa ardhi yao;
wakati maofisa serikali wanapotumia fedha kununua silaha badala ya kununua dawa;
wakati tabaka la juu ni wabadhirifu na mafisadi na masikini hawana pa kukimbilia-haya yote ni wizi na rabsha.
Huu kamwe si mwenendo unaoendana na Tao.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment