Monday, September 6, 2010

021

Mwalimu hupumzisha akili yake daima,
Sikuzote yuko pamoja na Tao;
hili ndilo linalompa nuru aliyokuwa nayo.

Tao huwa haikamatiki,
vipi akili zake ziwe pamoja na Tao.
Kwa sababu huwa hang'ang'anii dhana au wazo lolote liwalo.

Tao ni kiza na isiyo na mwisho,
Itamfanyaje yeye awe na nuru ?
Kwa sababu huiachia kufanya hivyo.

Kabla ya wakati na nafasi kuwepo,
Tao ipo.
Iko juu ya kuwa na kutokuwepo.
Ninajuaje hili ni kweli ?
Ni kwa kukiangalia kile kilicho ndani yangu nami nikakikubali.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment