Tuesday, September 7, 2010

014

Tazama, na hutakiona.
Sikiliza, na hutosikia kitu.
Jaribu kukikamata na hutoweza kukishika.

Kwa juu hakina mwangaza,
Kwa chini hakina kiza.
Bila umbo, bila jina
hatimaye hurejea katika milki ya kisichokuwepo.

Umbo linalojumuisha maumbo yote,
Taswira bila taswira,
Gumu kueleweka kupita ukomo wa dhahnia zote.

Kutana nayo na hutoona mwanzo wake;
ifuate na hutofika mwisho wake.
Huwezi ukaijua, lakini unaweza ukawa ndiyo yenyewe, bila kujua katika maisha yako ya kawaida ya kila siku.
Tambua tu kwanza ni wapi utokako
Hiki ndio kiini cha busara.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]

No comments:

Post a Comment