Palikuwa na kitu kisichokuwa na umbo na kilichokuwa safi kabisa kabla ulimwengu haujazaliwa.
Ni tulivu. Tupu. Pweke. Isiyobadilika. Isiyo na idadi.Inayokuwepo milele. Ni mama wa ulimwengu.
Kwa kukosa jina lingine linalofaa zaidi,
nimeamua kuiita Tao.
Hutembea katika kila kitu, nje na ndani na kisha hurudi kwenye asili ya vitu vyote.
Tao ni muhimu.
Ulimwengu ni muhimu.
Ardhi ni muhimu.
Mtu ni muhimu.
Hizi ndizo nguvu kuu nne muhimu maishani.
Mtu huifuata ardhi,
na ardhi huufuata ulimwengu
Na ulimwengu unaifuata Tao,
Wakati Tao hujifuata yenyewe tu.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Monday, September 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment