Sunday, September 5, 2010

058

Nchi inapotawaliwa kwa uvumilivu mkubwa,
Watu hustarehe na huwa waaminifu.
Nchi inapotawaliwa kwa kuwakandamiza watu na kuwaficha ukweli watu hukata tamaa na huwa wajanja kupita kiasi.

Uchu wa madaraka na kutaka kutawala unapokithiri,
Na malengo na matarajio yanapokuwa makubwa, basi na matokeo kiufanisi huwa sawa na hamna.
Jaribu kutengeneza mazingira ya watu kuwa na raha na furaha,
Kama hutakuwa unajenga msingi wa dhiki na matatizo chungu nzima.
Jaribu kufanya watu wawe watakatifu,
Na hujenga msingi wa jamii ya watu waovu, wezi na wazinzi.

Kwa hiyo Mwalimu huwa mtu anayetosheka kuwa mfano kwa wengine bila ya kutaka ukuu.
Ana ncha kama mkuki lakini hatoboi kitu.
Kanyooka, lakini teketeke.
Ana nuru kali, lakini hayaumizi macho ya watu.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment