Wanaojua huwa hawasemi.
Wanaozungumza sana huwa hawajui.
Funga mdomo wako,
zitie ganzi hisia zako,
Tia ubutu makali yako,
Yafungue mafundo yako
Lainisha mtazamo wako,
Ketisha chini vumbi lako,
Huu ndio utambulisho wa msingi.
Kuwa kama Tao.
Hauwezi kuifuata wala huwezi kuikimbia,
Kunufaika au kudhurika,
kutukuzwa au kudhalilishwa,
Huwa yajitolea mhanga wakati wote.
Ni kutokana na hili ndio maana hudumu milele.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment