Sunday, September 5, 2010

051

KIla kiumbe ulimwenguni ni taswira ya Tao.
Huwa hai ghafla
bila kujijua, iliyokamilika na huru.
Kisha huchukua umbo la kiumbe na kisha kuachia mazingira kuikamilisha.
Ni kwa sababu hii ndio maana kila kiumbe huitukuza Tao papo kwa hapo kinapozaliwa.

Tao ndio inayozaa viumbe wote,
Huwalisha,
Huwakimu, Huwatunza, Huwaliwaza, Huwalinda, na huwarudisha kwake yenyewe, huumba bila kumiliki, hufanza bila kutarajia, huongoza bila kuingilia.
Hii ndiyo sababu mapenzi kwa Tao yamo katikati ya asili ya kila kitu.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment