Monday, September 6, 2010

020

Acha kufikiri, umalize matatizo yako.
Nini tofauti kati ya ndiyo na hapana ?
Nini tofauti kati ya kufanikiwa na kutofaulu ?
Je, ni lazima wewe uthamini wanavyothamini watu wengine ?
Uepuke kile wengine wanachotaka kukiepuka ?
Uzandiki ulioje huu ?

Watu wengine wanasisimka kama vile wako kwenye gwaride.
Mimi peke yangu ndiye nisiyejali,
Mimi mwenyewe ndiye nisiyeonesha ishara yoyote,
kama vile mtoto mchanga kabla hajatabasamu.

Watu wengine wana kila kitu wanachokihitaji;
Mimi peke yangu ndiye nisiye na chochote.
Mimi peke yangu ndiye ninayetangatanga,
kama vile sina kwangu.
Ni kama mpumbavu, akili yangu haina kitu.

Watu wengine wote wanang'ara
Isipokuwa mimi peke yangu ndiye mwenye weusi wa giza.
Watu wengine wamenolewa,
mimi peke yangu ndiye butu.
Watu wengine wana sababu, mimi peke yangu ndiye nisiyejua.
Ninaelea kama wimbi baharini,
Ninavuma bila lengo kama upepo uvumavyo.

Ni tofauti na binadamu wa kawaida,
Ninanyonya kutoka matiti ya mama wa mama wote.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment