Sunday, September 5, 2010

055

Yule anayeoana na Tao ni kama vile mtoto mdogo aliyezaliwa jana.
Mifupa yake ni laini, na musuli zake ni dhaifu
lakini kamata yake ina nguvu ya kutisha.
Huwa hakajui lolote kuhusu kujamiana, lakini la kushangaza ni kwamba kaboo kake husimama,
Ana uwezo wa ajabu na unaotisha kiasi ambacho aweza kwa siku nzima kulia na kutoa kelele inayosikika mbali sana,
Lakini sauti yake haikauki
Utulive wake umekamilika mno.

Uwezo na nguvu ya gwiji ni kama hivi:
Huviachia vitu na watu wote waje kwake na kisha waondoke bila kuwa na matamanio yoyote.
Huwa hategemei matokeo
kwa hiyo hawezi akasikitika.
Kwa kuwa si mtu wa kusikitika basi huwa utu wake hauzeeki kamwe.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment