Saturday, September 4, 2010

068

Mwanariadha bora
hupenda mshindani wake awe katika kiwango chake cha juu.
Jemadari bora huingia akilini kwa adui yake.
Mfanyabiashara mkubwa na anayefanikiwa sana huwa anatumikia maslahi ya jamii yake.
Na kiongozi bora huwa anafuata matakwa ya wale anaowaongoza.

Wote huwa wanaenzi maadili ya kutokuwa na ushindani.
Sio kwamba hawapendi kushindana,
ila hushindana katika mazingira ya kimchezo na utani.
Katika hili hakika ni sawa na watoto
na hawapingani kabisa na Tao.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment