Monday, September 6, 2010

037

Tao huwa haifanyi kitu chochote,
lakini kupitia kwake vitu vyote hufanyika.

Kama wanawake na wanaume wenye nguvu wangeliweza kujiweka ndani yake,
Dunia nzima itabadilika yenyewe katika mdundo wake wa kawaida.
Watu wataridhika na maisha yao ya kawaida ya kila siku, katika maridhiano na bila matamanio yoyote.

Pakiwa hakuna matamanio basi dunia yote huwa katika amani.


AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment