Kutawala nchi kubwa
Ni sawasawa na kukaanga samaki mdogo.
Humharibu samaki kwa kumgusa gusa sana.
Iweke nchi yako katikati ya Tao
Na maovu hayatakuwa na mwanya.
Sio kwamba kwa sababu maovu hamna
Ila ni kutokana na ukweli kwamba utaweza kuyakwepa kirahisi.
Usiachie uovu ushindane na mtu au kitu chochote
Na wenyewe hatimaye utatoweka.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Saturday, September 4, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment