Mtu bora anaposikia kuhusu Tao,
Hapo hapo huanza huikumbatia.
Mtu wa kawaida anaposikia juu ya Tao,
huamini nusu, na nusu huishuku.
Mtu mjinga anaposikia kuhusu Tao,
Hucheka kicheko kikubwa,
Kama asingelicheka, basi hii isingelikuwa ni Tao.
Ndio maana husemwa:
Njia ya kwenda kwenye mwanga huonekana ni yenye kiza,
Na njia inayompeleka mtu mbele aghalabu honekana kurudi nyuma,
Njia iliyonyooka huonekana refu,
Nguvu huonekana unyonge,
Utakatifu huonekana uchafu,
Kutobadilika huonekana kuwa kitu kinachowezekana kubadilika,
Uwazi huonekana kitu kilichofichika,
Mashuhuri huonekana watu wa kawaida,
Pendo kubwa na lisilo na ukomo huonekana kutokujali,
Na hekima iliyo kubwa huonekana kama mambo ya kitoto.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment