Tuesday, September 7, 2010

016

Toa mawazo yote katika akili yako.
Acha moyo wako uwe katika amani.
Angalia misukosuko ya viumbe, lakini tafakari kurudi kwao.

Kila kiumbe katika dunia hii hurudi kwenye asili yake.
Kurudi kwenye chanzo chako ni utulivu.

Ikiwa hukijui chanzo chako basi huweweseka katika mtafaruku na huzuni.
Unapofahamu ni wapi unakotoka hujikuta mvumilivu, usiyevutwa na lolote, unayeshangazwa na mwenye moyo wa huruma kama nyanya,
mtukufu kama mfalme,
ukijitumbukiza katika maajabu ya Tao,
unaweza kupambana na lolote maisha yanachokuletea, na kifo kikija kinakukuta uko tayari.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]

No comments:

Post a Comment